
ZUIA WAFUATILIAJI
Tor Browser inatenganisha kila tovuti unayotembelea kwahiyo wadukuzi wasiohusika mojakwamoja na matangazo hayawezi kukufuata. Vidakuzi vyovyote mojakwamoja vitafutika baada ya kumaliza kuperuzi. Kwahiyo historia yako ya kuperuzi pia itafutika.

KUJILINDA DHIDI YA UCHUNGUZI
Tor Browser huzuia mtu kuona mawasiliano yako yaa tovuti unayoitembelea. Wote wanaofuatilia shughuli zako mtandaoni wataweza kuona unatumia Tor.

WEKA UPYA FINGERPRINTING
Tor Browser inalenga kufanya watumiaji wote kuwa sawa, kufanya ugumu kwa mmoja kutambulika kutokana na taarifa za kivinjari na kifaa chako unachotumia.

USIMBAJI WA MATABAKA ZAIDI YA MOJA
Usafirishwaji wa data zako upo katika matabaka na umesimbwa mara tatu unapopita katika mtandao wa Tor. Mtandao una maelfu ya watu wanaojitolea kusimamia seva zinazofahamika kama Tor relays.

PERUZI BURE
Pamoja na Tor Browser, una uhuru na kupata tovuti ambazo mtandao wako umezizuilia.
kuhusiana na sisi
tunaimani kila mtu anapaswa kuweza kutumia mtandandao kwa faragha. Sisi ni mradi wa Tor, shirika lisilo la faida la Marekani lenye hadhi ya 501(c)(3). tunaboresha haki za binadamu na kulinda faragha yako mtandaoni kupitia programu ya bure na mtandao wazi. Pata kujua timu yetu.